Umati wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mshiriki namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya fainali.
Mshiriki namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia hatua ya fainali.
Shindano la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka wageni waliohudhuria na kujikuta wakiimba kwa hisia.
Mshiriki Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahiri wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.
Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.
Kiongozi wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016 lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbi wa Milado, Sinza jijini Dar es Salam.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog.