moto shinyanga
Benki ya NMB Manonga mjini Shinyanga imenusurika kuungua moto baada ya jengo lililopo jirani na benki hiyo mali ya bwana Mohammed kuteketea kwa moto. 

Jengo lililoteketea kwa moto lipo katika mtaa wa Miti Mirefu  karibu naBenki ya NMB Manonga na sheli ya mafuta mjini Shinyanga. 

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo uliibuka jana Septemba 20,2016 majira ya saa moja jioni huku chanzo kikielezwa kuwa ni mtungi wa gesi ulikuwa jikoni.

Hata hivyo Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyangalikishirikiana na wadau mbalimbali lilifanikiwa kuzima moto huo majira ya saa tatu na nusu usiku na kufanikiwa kuokoa mali zilizokuwa katika robo tatu ya jengo hilo lililopo karibu na sheli ya mafuta pamoja na kuzuia madhara yasitokee kwenye benki ya NMB.

Inaelezwa kuwa robo ya jengo hilo imeungua na vitu vilivyokuwemo navyo vimeungua katika robo ya jengo hilo na kwamba hakuna majeruhi na hasara iliyopatikana bado haijajulikana 
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Karibu tena katika blog hii

 
Top